Jumuiya ya Wazazi CCM yamchangia Rais Mwinyi fedha ya fomu ya urais

 

BARAZA Kuu la Jumuiya ya Wazazi Tanzania la Chama Cha Mapinduzi (CCM) limempongeza na kumchangia Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Rais wa Zanzibar ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, fedha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuchukulia fomu ya kugombea urais wa Zanzibar kutumikia wananchi kwa miaka mingine mitano.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Ndugu. Fadhil Maganya (MCC) wakati wa Kongamano la Kumpongeza Rais Dkt. Hussein Mwinyi kwa kutimiza miaka minne pamoja na utekelezaji mkubwa wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2020 - 2025 ikiwemo ujenzi wa barabara mijini na vijijini, ujenzi wa masoko ya kisasa, uwekezaji katika sekta ya michezo pamoja na kuboresha kwa Uwanja wa New Amani Complex, Ujenzi wa Shule za gholofa zaidi ya 20 ambazo zimekashamilika na pia serikali ina mpango wa kuongeza shule nyingine za gholofa zaidi ya 30 pamoja na miradi mingine ya kimkakati ikiwemo sera yake ya uchumi wa buluu.

"Mheshimiwa Rais Dkt.Hussein Mwinyi, kwa kauli moja sisi wajumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi wa CCM kwa pamoja katika kikao chetu cha Baraza Kuu Maalumu cha Jumuiya ya Wazazi kilichokaa jana tuliazimia kukuchangia fedha shilingi milioni moja,” amesema Ndugu Mganya.

Chapisha Maoni

0 Maoni