Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania
(TANAPA) ladhamini na kushiriki Maonesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar 2024
(Zanzibar Tourism and Investment Show 2024) yanayofanyika Dimani- Fumba
Visiwani Zanzibar.
Licha ya kuwa Mdhamini Mkuu wa Maonesho
hiyo tumepata fursa ya kuungana na wadau wa Utalii, wawekezaji mbali mbali
kutoka Zanzibar katika ufunguzi wa Maonesho hilo ambalo Mgeni Rasmi ni Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi, imesema taarifa ya TANAPA
Uwakilishi wa Shirika ulifanywa na
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara, Jully Lyimo (kwa niaba
ya Kamishna wa Uhifadhi) ambapo alipata fursa ya kutoa neno la shukrani.
"Kama Shirika, tutaendelea kushirikiana
na wadau wa Sekta ya Uhifadhi na Utalii katika kutangaza Utalii, fursa za
Uwekezaji katika Hifadhi za Taifa Nchini pamoja na kutoa elimu ya Uhifadhi" amesema Lyimo.
Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar 2024 (Zanzibar Tourism and Investment Show 2024) yanayofanyika Dimani- Fumba Visiwani Zanzibar, Oktoba 25-26 2024.
0 Maoni