Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
(NCAA) inashiriki Maonesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar yanayofanyika kuanzia
tarehe 25 na 26 Oktoba 2024, Dimani, Fumba, Zanzibar.
Katika maonyesho hayo, NCAA inatangaza
fursa za uwekezaji katika miradi ya utalii na miundombinu ndani ya hifadhi.
Vivutio vya kipekee kama Kreta ya
Ngorongoro, Bonde la Olduvai, na Eneo la Ndutu vinavutia wawekezaji na
kuimarisha nafasi ya Tanzania kwenye ramani ya utalii wa kimataifa.
NCAA pia inatoa elimu kwa washiriki
kuhusu uhifadhi wa maliasili na umuhimu wa urithi wa dunia, ikiwahamasisha
kuunga mkono uhifadhi shirikishi unaolenga kulinda na kuboresha mazingira ya
hifadhi. Washiriki wanajifunza mikakati endelevu inayotekelezwa na NCAA ili
kulinda maeneo haya muhimu.
Maonyesho haya ni jukwaa muhimu kwa
NCAA kuwahamasisha wawekezaji kushirikiana nao katika miradi ya uhifadhi na
utalii, ili kuchangia katika uchumi wa taifa na kuhakikisha kuwa urithi wa
Tanzania unadumu kwa vizazi vijavyo.
0 Maoni