Serengeti, Mlima Kilimanjaro zatwaa tuzo za Afrika

 

Tanzania imeibuka kidedea kwa hifadhi zake mbili kushinda tuzo za vivutio bora barani Afrika, ambapo tuzo ya Hifadhi Bora barani Afrika 2024 ikichukuliwa na Serengeti na tuzo ya kivutio bora barani Afrika ikitwaliwa na Mlima Kilimanjaro.

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo zilifanyika jana usiku Oktoba 14, 2024 huko Mombasa nchini Kenya ambapo TANAPA walizifuatilia tuzo hizo mubashara katika viwanja vya Makao Makuu ya TANAPA yaliyopo jijini Arusha, Tanzania.

TANAPA walifuatilia hafla za utoaji tuzo hizo za mwaka huu hatua kwa hatua wakiongozwa na Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Musa Nassoro Kuji, akiwa pamoja na maafisa wengine.

Hifadhi ya Serengeti imeshinda tuzo hiyo ya Hifadhi Bora Barani Afrika kwa mara sita mfululizo kuanzia mwaka 2019 mpaka sasa.

Huku, Mlima Kilimanjaro ukishinda tuzo hiyo ya Kivutio Bora Barani Afrika mwaka 2013, 2015, 2016, 2017, 2018, na sasa 2024 ikiwa ni mara sita.





Chapisha Maoni

0 Maoni