Mume amuua mkewe kwa kisu, kisha naye kujiua

 

Mwanaume mmoja Mkoani Songwe amemuua kwa kumchoma na kisu mkewe aliyekuwa ametengana naye kwa muda na kisha naye kujiua kwa kujichoma na kisu tumboni.

Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Songwe ACP Johnny Maro amemtaja mwanaume huo kuwa ni Ally Joseph Mwakilembe (45) Mkazi wa Kijiji ha Kapeta Kata ya Ikinga Tarafa ya Bundali Wilayani Ileje.

Kamanda Maro amesema Mwakilembe alimuua mkewe Wema Angolile Ndile (32) kwa kumchoma na kisu sehemu za shingoni na upavuni upande wa kulia akiwa nyumbani kwake na kumsababishia kifo.

Baada ya kufanya tukio hilo Oktoba 15, 2024 majira ya saa 4:30 usiku Mwakilembe naye alijichoma kwa kisu tumboni na alikimbizwa hospitali ya Wilaya ya Ileje, ambapo alifariki dunia Oktoba 17, 2024 saa 9:30 alfajiri.

Ally Joseph Mwakilembe na Wema Angolile Ndile walikuwa mke na mume na walitengana miezi mitano iliyopita ambapo mke aliamua kwenda kuishi sehemu nyingine, imesema taarifa hiyo.

Kamanda Muro amesema kwamba uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi. Jeshi la Polisi limeitaka jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.

Chapisha Maoni

0 Maoni