Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema
kila mwaka kuna wagonjwa wapya milioni 2.3 wa Saratani ya matiti
wanaogundulika duniani.
WHO imetoa taarifa yake hiyo katika
mwezi huu wa Oktoba ambao hutumika katika kuwaelimisha watu duniani kuhusiana
na Saratani.
Taarifa hiyo ya WHO imesema nusu ya wanawake wanaougua Saratani
huwa hawana dalili za kuwa katika hatari za kuugua ugonjwa huo, bali ni kwa
kuwa ni wanawake ama kuzeeka.
Kupunguza vifo vya Saratani na matiti
kwa asilimia 2.5 kwa mwaka kunaweza kudhibiti asilimia 25 ya vifo ifikapo 2030
na asilimia 40 ifikapo mwaka 2040 kwa wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 70.
Saratani ya matiti ni ugonjwa unaosababishwa
na seli zisizozakawaida zinazokua na kushindwa kudhibitiwa na kisha kugeuka
kuwa uvimbe kwenye matiti.
Iwapo mtu anayeugua Saratani ya matiti
asipofanyiwa uchunguzi uvimbe huo utasambaa mwilini na kuhatarisha maisha.
0 Maoni