Mchechu aipongeza TAWIRI, ahimiza ubunifu katika kujiendesha

 

Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kwa shughuli za utafiti wa Wanyamapori ambazo zina tija katika sekta ya uhifadhi na utalii ambayo inachangia asilimia 17% ya pato la Taifa.

Akizungumza jana Oktoba 21, 2024 wakati wa kikao na Menejimenti ya TAWIRI, Bw. Mchechu amesema Ofisi ya msajili wa Hazina itaendelea kushauri vyema katika kuimarisha Mashirika ya Umma yaweze kujiendesha kwa tija.

“Nawapongeza kwa utendaji mzuri, nitoe wito kuendelea kuwa wabunifu kutumia rasimali mlizo nazo kujiendesha kwa ufanisi,” amehimiza  Bw. Mchechu.

Naye, Mkurugenzi Mkuu TAWIRI Dkt, Eblate Mjingo amesema TAWIRI ni taasisi ya kimkakati  ambayo mbali na kutokuonekana  ikizalisha  fedha moja kwa moja ina mchango  mkubwa katika mapato yatokanayo na utalii nchini ambapo takwimu na taarifa za tafiti ndizo zinazonadi utalii na kuimarisha uhifadhi.




Chapisha Maoni

0 Maoni