Ajali ya nyumbani yamkosesha Rais Lula safari ya Urusi

 

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amesitisha safari yake ya kwenda Urusi baada ya kuumia kichwani katika ajali iliyotokea nyumbani siku ya Jumamosi.

Lula mwenye umri wa miaka 78, alikuwa asafiri sku ya jumapili alasiri kushiriki mkutano wa Jumuiya ya Nchi Zinazoendelea za Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini (BRICS)

Hospitali Kuu ya ya Mji wa Brasilia imemshauri Rais Lula, kujiepusha na safari ndefu za ndege kwa muda.

Kutokana na hali hiyo Lula sasa itabidi ashiriki mkutano huo wa BRICS kwa njia ya mdandanoni ya mkutano kwa njia ya video.

Chapisha Maoni

0 Maoni