Maseneta Kenya wamuondoa Madarakani Naibu Rais akiwa hospitali

 

Maseneta wamepiga kura ya kumuondoa madarakani Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua ofisini licha ya kushindwa kutoa ushahidi wake katika kesi ya kumuondoa madarakani baada ya wakili wake kusema kuwa ni mgonjwa na amepelekwa hospitalini.

Katika hali ya kushangaza katika historia ya nchi hiyo kisiasa, Gachagua alipaswa kufika katika Seneti baada ya chakula cha mchana kujitetea, siku moja baada ya kukanusha mashtaka 11.

Hata hivyo, Gachagua, almaarufu Riggy G, hakufika na wakili wake akaomba kuahirishwa akisema mteja wake alikuwa akisumbuliwa na 'maumivu ya kifua' na alikuwa akitibiwa na madaktari katika Hospitali ya The Karen.

Baada ya Gachagua kushindwa kutokea, kulitokea mvutano wa kuhairishwa kwa kikao hicho hata hivyo Maseneta waliamua kuendelea na kesi bila yeye kuwepo, na hivyo kusababisha timu ya mawakili wake kuondoka katika chumba hicho.

Kura za Maseneta hao wa Kenya dhidi ya mashtaka 11, zimehitimisha harakati za Gachagua kujitetea kwa upande wa ngazi za kisiasa, ambapo sasa amebakiza hatua ya kwenda Mahakamani iwapo anataka kupinga uamuzi huo.


Chapisha Maoni

0 Maoni