Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kutoka Mlima Kilimanjaro

 

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu akipokea kikosi maalumu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kilichopandisha Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro leo tarehe 21-10-2024 katika Lango la Marangu linalotumika kwa ajili ya kupandia na kushukia watalii lililopo Mkoani Kilimanjaro.

Mapokezi ya awali ya Kikosi hicho yaliongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Jacob Mkunda.



Chapisha Maoni

0 Maoni