CDF Mkunda awasili Kilimanjaro kupokea Mwenge

 

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda, tayari amewasili katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro tayari kwa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Jenerali Mkunda amepokelewa leo tarehe 21, Oktoba 2024 na mwenyeji wake Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Musa Nassoro Kuji.

Ikumbukwe kuwa tarehe 14, Oktoba 2024 Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi la Ulinzi na Usalama Rais Samia Suluhu Hassan alimkabidhi Mwenge wa Uhuru na Bendera Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda, ili Jeshi hilo liupeleke kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya sherehe za miaka 60 tangu kuanzishwa kwa mbio za mwenge huo.

Ambapo tarehe 15, Oktoba 2024 Kikosi maalumu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kilianza safari ya kupandisha Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.



Chapisha Maoni

0 Maoni