Waokoaji kusini mwa Hispania
wanafanyakazi bila ya kuchoka kutafuta iwapo bado kuna mtu yeyote aliyepotea baada
ya mafuriko yaliyoua watu wapatao 95.
Haijafahamika hadi sasa idadi ya watu
ambao hawajapatikana, lakini mamia ya wanajeshi wamepelekwa huko Valencia kusaidia,
eneo moja wapo lililoathirika mno.
Baadhi ya maeneo yanaweza kufikika kwa
helkopta tu, kutokana na barabara kujaa matope zito, vifusi na magari yaliyopandiana.
0 Maoni