Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani amejiandikisha kwenye
daftari la wakazi katika mtaa wa Chimuli II kwenye kituo cha Shule ya Msingi
Chadulu jijini Dodoma leo Oktoba 19, 2024.
Akizungumza baada ya kujiandikisha,
Bw. Kailima aliwasisitiza wananchi umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kuandikishwa
katika maeneo yao ili watimize haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.
"Nimetoka kujiandikisha katika
orodha ya wakazi ambayo itazaa daftarinla orodha ya wapiga kura kwaajili ya
uchaguzi wa serikali za mitaa, niwaombe na kuwasihi wananchi wote wenye umri wa
miaka 18 na wenye sifa za kuandikishwa wajitokeze kuandikishwa ili watumie haki
yao ya kikatiba ya kupiga kura.”
Kailima amesema watu wa makundi yote,
Wazee, wakina mama na vijana wenye sifa wajitokeze kwani imesalia siku moja ili
kuhitimisha zoezi hilo kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Aidha amesema vituo vipo katika maeneo
mbalimbali yaliyo karibu na makazi ya wananchi hasa katika mashule na ofisi za
mitaa.
Uandikishaji wa wapiga kura wa
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kwenye daftari la wakaazi, ulianza tarehe 11
Oktoba, 2024 na utamalizika tarehe 20 Oktoba 2024.
Wananchi waliojiandikisha watapiga
kura kuchagua viongozi wa mitaa na vijiji Novemba 27, 2024 katika uchaguzi wa
serikali za mitaa.
0 Maoni