Gachagua atinga Mahakamani kesi ya kupinga kuenguliwa

 

Mahakama ya Sheria ya Milimani iliyopo jijini Nairobi nchini Kenya inaendelea kusikiliza kesi ya kuenguliwa madaraka na Seneti, Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua

Gachagua aliwasili mahakamani akiwa na wanasiasa wanaomuunga mkono, akiwamo aliyekuwa Katibu Mkuu wa UDA Cleophas Malala, Gathoni Wamuchomba, Njeri Maina, pamoja na Mbunge wa Embakasi ya Kati Benjamin Gathiri, na wengineo.

Kesi hizo mbili, moja yakupinga kuenguliwa Gachagua, na nyingine kuapishwa kwa mrithi wake, zinasikilizwa na jopo la majaji Fredah Mugambi, Eric Ogola pamoja na Anthony Mrima.

Katika kesi hizo upande wa Gachagua unawakiliswa na Wakili Mwandamizi Paul Muite, akishirkiana na Elisha Ongoya, Ndegwa Njiru, pamoja na mawakili wengine.

Chapisha Maoni

0 Maoni