Gachagua alia kuondolewa ulinzi akiwa hospitali

 

Naibu Rais wa Kenya aliyeondolewa wadhifa wake na Baraza la Seneti la Kenya, Rigathi Gachagua, ametoka hospitali leo na kulalamika kuondolewa walinzi wake akiwa amelazwa hospitali.

Gachagua akiongea nje ya hospitali aliyolazwa amesema,"Nibahati mbaya wakati nikiwa hapa hospitali, kaka yangu na rafiki yangu Rais William Ruto ameagiza niondolewe ulinzi."

Amesema kwamba licha ya yeye kuondolewa ulinzi hospitali, pia walinzi waliokuwa nyumbani yake ya Karen Jijini Nairobi na nyumba ya kwao Nyeri pia wameondolewa.

Kama hiyo haitoshi, Gachagua amedai kuwa watumishi wote waliokuwa kwenye Ofisi Naibu Rais wamepewa likizo ya dharura na magari yote yaserikali yamechukuliwa.

Gachagua amesema anashangaa kufanyiwa hayo yote na Rais William Ruto wakati akijua kwamba Mahakama imetoa zuio la uamuzi wa kuenguliwa kwake madarakani na Baraza la Seneti.

Chapisha Maoni

0 Maoni