Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa
Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Oktoba 21, 2024 akiwa nchini Singapore
amekutana na kufanya mazungunzo na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini
humo, Bw. Teo Siong Seng ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Kampuni ya Pacific
International Lines (Pte) Ltd.
Katika mazungumzo yao, Dkt. Biteko
amesema kuwa Serikali inathamini kazi ya uwakilishi inayofanywa na Bw. Seng na
kuwa itaendelea kumpa ushirikiano katika kutekeleza jukumu hilo.
Pia, ameikaribisha sekta binafsi kwa ajili
ya kuwekeza katika sekta ya nishati ili kuongeza kasi ya uzalishaji,
uunganishaji na usambazaji wa nishati nchini Tanzania.
Kwa upande wake, Bw. Seng ameishukuru
Serikali kwa kumpa fursa hiyo ya kuiwakilisha Tanzania nchini Singapore huku
akiahidi kuendelea na jukumu hilo ikiwa ni pamoja kutangaza utalii.
Dkt. Biteko yuko nchini Singapore kwa
ajili ya kushiriki Mkutano wa 17 wa Wiki ya Kimataifa ya Nishati ambao unalenga
kuwakutanisha wadau wa sekta hiyo kwa ajili ya kujadili mahitaji ya nishati
yanayoongezeka duniani ikiwa ni pamoja na kuharakisha juhudi za kupunguza hewa
ya ukaa.
0 Maoni