Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Makalla na Mlezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam amezungumza hayo wakati wa hafla ya kupokea taarifa ya zoezi la uandikishaji wa daftari la mkazi la uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mkoa wa Dar es Salaam, taarifa aliyoipokea kutoka kwa viongozi wa CCM wa mkoa huo leo, Jumanne Oktoba 22.2024
Nianze kuwapongeza Viongozi wa CCM
kuanzia ngazi Mkoa mpaka Mabalozi pamoja na Wafuasi wa CCM na Wananchi kwa
Ujumla yaani Mkoa mzima wa Dar es salam kwa kutoa Ushirikiano katika zoezi zima
la Uandikishaji mpaka kufikia asilimia 96.7 hii ni faraja kwa CCM kwani Dar es
salam ni uso wa Nchi.
Awamu hii Wananchi wamejiandikisha kwa
wingi sana na hii imechagizwa na Utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM
hilo halina kificho kwa sababu miradi haitekelezwi hewani, Miradi ya Zahanati,
Madarasa, Vituo vya Afya imetekelezwa kwenye Vijiji na Vitongoji hivyo Wananchi
wameona kazi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.
CPA Makalla amesema endapo chama hicho
tawala hapa nchini kitapoteza kwenye baadhi ya vitongoji, vijiji au mitaa
vitaheshimu matokeo hayo na kwamba huo utakuwa wakati muafaka kwao kujitafakari
na kujipanga kwa nini walipoteza eneo hilo, ili uwe njia ya kufanya vizuri
kwenye uchaguzi ujao.
Mwisho Mwenezi Makalla amesisitiza CCM
haihitaji mbeleko kwani kwa takwimu tulizopokea ndani ya Chama na zile za
Wizara ya Tamisemi kwani Maandalizi yaliyofanyika na Viongozi wa CCM wote na
Jumuiya Kwa kazi nzuri na kuleta taswira ya Ushindi wa kishindo.
0 Maoni