Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana
(Mb) amesisitiza kuwa zoezi la kuhama kwa hiari kwa wananchi wa Ngorongoro
linaendelea huku akisisitiza kwamba Serikali inafanya maboresho mbalimbali ili
kurahisisha zoezi hilo.
Dkt. Chana ameyasema hayo jana Septemba 12, 2024 alipokuwa
akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro katika
Makao Makuu ya Ofisi za NCAA Wilayani Karatu Mkoani Arusha.
"Niseme tu kwamba zoezi la kuhama kwa hiari
linaendelea na maboresho yanaendelea na
kuna maeneo ya Kitwai, Kilindi na sehemu nyingine ambazo watu wanapenda kwenda
wanaenda kwa hiari " amesisitiza Mhe. Chana.
Amewataka Askari Uhifadhi kusimamia vyema zoezi hilo ili
kurahisisha utekelezaji wake.
Aidha, amewataka kuendelea kufuata maelekezo mbalimbali ya Serikali ikiwa ni pamoja na kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi kama geti na vyoo vya wanafunzi.
0 Maoni