Uwepo wa SGR unaashiria utoshelevu wa umeme- Dkt. Biteko

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema safari za treni za reli ya kisasa (SGR) zinazotumia umeme kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ni ushahidi kuwa Tanzania ina umeme wa kutosha.

Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Septemba 12, 2024 baada ya kuwasili jijini Dodoma akitokea Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa treni ya mwendo kasi (SGR) kwa mara ya kwanza.

"Safari za treni ya umeme ya SGR ni ushahidi mwingine kuwa nchi ya Tanzania ina umeme wa kutosha, ni ushahidi mwingine kwamba nishati ya umeme ikipatikana ya uhakika inafungua fursa mbalimbali za kiuchumi, viwanda mbalimbali vinajengwa na kongani za viwanda kuongezaka,”amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha umeme unatosheleza Wizara ya Nishati kazi yake ni kuhakikisha kuwa umeme unakuwapo wa kutosha wakati wote ili huduma hizi ziweze kuendelea kupatikana kwa Watanzania bila matatizo.



Chapisha Maoni

0 Maoni