Machifu
nchini wamepongezwa kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuungana na Serikali
chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
katika Kuimarisha amani na Utulivu nchini.
Pongezi hizo
zimetolewa leo Septemba 22,2024 na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi,
Dkt. Pindi Chana (Mb) aliyeambatana na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi Mkoani Ruvuma alipokutana
na Machifu kutoka makabila mbalimbali ya hapa nchini waliofanya ziara ya
kutembelea Makumbusho ya Historia ya Vita vya MajiMaji Mjini Songea kama sehemu
ya Maandalizi ya mapokezi ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa
kuitembelea Makumbusho hiyo hapo kesho.
Mhe. Chana
aliwahakikishia Machifu hao kuwa Wizara anayoingoza itaendelea kushirikiana
nao kikamilifu katika Uhifadhi na
kuendeleza urithi wa Kihistoria nchini ili watanzania waweze kunufaika na Mazao
hayo ya Utalii wa Historia na Malikale.
Pamoja na
kukutana na Machifu hao, Mhe. Balozi Chana amekagua maandalizi ya mapokezi ya
Mhe. Rais Samia kwenye Makumbusho hiyo iliyohifadhi Historia adhimu na adimu
katika ukombozi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla dhidi ya Ukoloni Miaka
takribani 119 iliyopita.
0 Maoni