Kuanzia
Oktoba mosi mwaka huu, mchimbaji ama mfanyabiashara wa dhahabu anayetaka
kusafirisha dhahabu nje ya nchi, anapaswa kutenga asilimia 20 ya dhahabu yote
anayotaka kusafirisha nje, kwa ajili ya kuiuzia Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Taarifa
iliyotolewa na Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Madini Mhandisi Ramadhani Lwamo
imesema kiasi hicho cha asilimi 20 ya dhahabu kinapaswa kuwasilishwa katika
viwanda vya kusafisha dhahabu (refineries) vya Eyes of Africa Ltd cha Dodoma na
Mwanza Precious Metals Refineary Ltd cha Mwanza.
Taarifa hiyo
imesema kwamba taratibu za malipo ya dhahabu hiyo ya kiwango cha asilimia 20 ya
dhahabu itakayouzwa nje, zitafanywa kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania. Takwa
hili ni kwa mujinu wa kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini, Sura ya 123.
Utaratibu
huu unakuja kufuatia kupitishwa kwa Muswada wa Fedha wa Mwaka 2024/2025 na
Bunge la Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, ambapo Sheria ya Madini inamtaka kila
mchimbaji ama mfanyabishara wa madini kutenga asilimia 20 ya dhahabu
inayozalishwa kwa ajili ya kuiuzia BoT, kabla ya kuisafirisha nje ya nchi.
0 Maoni