Wamarekani changueni “shetani mwenye nafuu”- Papa Francis

 

Papa Francis amesema wagombea wote wawili wa Marekani wanapinga uhai, na kuwashauri wapigakura Wakatoliki kumchangau shetani mwenye nafuu, wanapopiga kura Novemba.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani amesema kutowakaribisha wahamiaji akimlenga Trump ni kosa kubwa, na kufananisha msimamo wa Kamala Harris wa utoaji mimba sawa na uaji.

“Wote wanapinga uhai, iwe kwa anayefukuza wahamiaji, ama kwa yule anayeua watoto,” Papa alisema katika kauli yake kuhusu siasa aliyoitoa Ijumaa akimaliza ziara yake ya siku 12 Kusini mashariki mwa Asia.

Hata hivyo Papa Francis hakutaja jina la Kamala Harris ama Donald Trump kwenye kauli zake.

Chapisha Maoni

0 Maoni