Rais wa Comoro shambuliwa kwa kisu msibani

 

Rais wa Comoro Azali Assoumani amejeruhiwa baada ya kushambuliwa wa kisu, mamlaka za nchi hiyo zimesema.

Taarifa ya msemaji wa serikali ya Comoro Fatima Ahamada imesema “Tunashukuru Mungu maisha yake hayapo hatarini.”

Assoumani alishambuliwa wakati akihudhuria maziko ya kiongozi wa kidini jijini Moroni lakini alijeruhiwa kidogo, alisema Ahamada.

Ahamada ameeleza kuwa mtu aliyemshambulia amekamatwa, ingawa bado haijajulikana wazi sababu za mshambuliaji kufanya tukio hilo.

Chapisha Maoni

0 Maoni