Uharibifu mkubwa wa misitu wachochea mabadiliko ya tabia nchi

Mabadiliko ya tabia nchi yanayotokea nchini Tanzania ni moja matokeo ya uharibifu wa mazingira ikiwemo uharibifu mkubwa wa misitu unaoendelea ambapo kwa sasa nchi inapoteza takriban hekta 469,000 za misitu kwa mwaka.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) alipokuwa akijibu swali la Mhe. Maryam Azan Mwinyi (Mb) aliyetaka kujua  mkakati wa Serikali wa kusimamia uhifadhi wa misitu hasa ikizingatiwa kwamba imeandaa na kuzindua biashara ya hewa ya ukaa.

Mhe. Kitandula alisema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kulinda misitu iliyopo na kuongeza upandaji miti nchini. Miongoni mwa  mikakati hiyo ni mkakati wa Kuongoa Misitu wa 2024, Makakati wa Mianzi 2024, Mwongozo wa Kitaifa wa Uandaaji na Utunzaji wa Kitalu cha Miche ya Miti wa 2024, Mkakati wa Kitaifa wa Kilimo Mseto wa 2024, Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034; pamoja na uimarishaji wa doria za mara kwa mara za kuzuia ukataji miti hovyo.

Na Anangisye Mwateba-Bungeni Dodoma.

Chapisha Maoni

0 Maoni