Bodi ya Ushauri wa Masuala ya Kazi yapongezwa

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhwani Jakaya Kikwete, amekutana na kufanya mazungumzo na kuwapongeza  Bodi ya Ushauri wa Masuala ya Kazi, Uchumi na Kijamii (LESCO) kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yao wanapoelekea kumaliza muda wao wa Miaka Mitatu ya Kazi.

Pamoja na kuwapongeza Mhe. Ridhwani, ametoa rai kwa wajumbe wa Baraza hilo kuendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuhakikisha sekta ya kazi na ajira inazingatia misingi ya kazi zenye staha kwa maslahi ya wafanyakazi na waajiri.

Awali, Mwenyekiti wa LESCO Dkt. Samwel Nyantahe, ameishukuru Serikali kwa kutoa ushirikiano katikia kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yao.

Uongozi wa Baraza hilo unamaliza muda wake Septemba 12, 2024 na kwa sasa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeanza mchakato wa kuwapata wajumbe wengine

Chapisha Maoni

0 Maoni