Mamlaka ya
Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imeshiriki katika maonesho na kongamano la maadhimisho ya siku ya utalii
duniani lililoanza tarehe 26/9/2024 na kufikia kilele 27/9/2024 katika hoteli
ya Gran Melia jijini Arusha.
TAWA ikiwa
ni sehemu ya wadhamini wa kongamano
hilo, imetumia nafasi hii kukutana na
wadau mbalimbali wa tasnia ya utalii
kuelezea vivutio adhimu ilivyonavyo katika maeneo inayosimamia pamoja
na fursa za uwekezaji katika maeneo
hayo.
Mgeni rasmi
katika kongamano hilo alikuwa ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dastan
Kitandula (Mb) aliyepongeza jitihada zinazofanywa na sekta binafsi katika kuuza
vivutio vya nchi yetu, alisisitiza mchango wa utalii katika uchumi wa nchi yetu
na kuelezea ni namna gani Serikali inaboresha miundombinu ya utalii pamoja na
kufungua soko la utalii kwa upande wa kusini mwa Tanzania.
Kongamano
hili limeandaliwa na Chuo Cha Uhasibu Arusha kwa kushirikiana na taasisi ya
Rethinking Tourism Africa likiwakutanisha
wadau wa sekta ya utalii kutoka ndani na nje ya Tanzania.
0 Maoni