Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza
na Princess Sophie (Duchess of Edinburgh) aliyepo Zanzibar kwa ziara ya siku
sita kutembelea miradi mbalimbali ya Afya inayotekelezwa na taasisi tofauti
ambazo yeye ni mlezi wake.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi amesema hatua iliyofikiwa na Zanzibar
ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali inatokana na juhudi kubwa na misaada ya
afya inayotolewa na Uingereza, na kumuahidi kuwa Zanzibar itaendelea kufanya
kazi kwa bidii ili kupambana na magonjwa, hasa yasiyoambukiza (NCDs),
yanayoathiri ustawi wa jamii.
Halikadhalika, Rais Dk. Mwinyi amemuhakikishia Princess
Sophie kuwa Zanzibar inaendelea kuweka mkazo zaidi na kuhakikisha huduma bora
za sekta ya afya, hususan kuimarisha huduma za kitengo cha uzazi salama cha
mama na mtoto, na kuwataka wafadhili pamoja na washirika wengine wa maendeleo
kuendelea kuiunga mkono Zanzibar.
Kwa upande mwingine, Princess Sophie ameipongeza Zanzibar
kwa hatua iliyofikia ya kudhibiti ugonjwa wa Trakoma kwa kiasi kikubwa na kufikia
mapema malengo yaliyowekwa na Jumuiya ya Madola (Commonwealth) ya kumaliza
ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.
Princess Sophie (Duchess of Edinburgh) ni mke wa mtoto wa mwisho wa aliyekuwa Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, Prince Edward, ambaye ni mdogo wa Mfalme wa sasa wa Uingereza, Charles III.
0 Maoni