Nyangumi ‘Jasusi wa Urusi’ akutwa amekufa kwenye fukwe Norway

 

Samaki aina ya nyangumi anayehisiwa kuwa amepatiwa mafunzo ya ujasusi na Urusi amekutwa amekufa kwenye fukwe huko Norway.

Mwili wa nyangumi huyo aliyepachikwa jina la Hvaldimir ulikutwa ukielea majini kwenye mji wa kusini magharibu wa Risavika na kuchukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Nyangumi huo Jajusi wa Urusi alionekana kwa mara ya kwanza kwenye maji miaka mitano iliyopita akiwa na kamera ya hali ya juu ya kunasa picha ikiwa na maneno “Kifaa cha St Petersburg".

Tangu hapo kukaibuka uvumi kuwa huenda ni nyangumi jasusi, suala ambalo wataalamu wanasema liliwahi kutokea huko nyuma. Hata hivyo Urusi haikusema lolote kuhusiana na madai hayo.

Askari wa kikosi cha wanamaji Sebastian Strand aliambia shirika la habari za AFP chanzo cha kifo cha nyangumi huyo hakijajulikana kutokana na kukutwa akiwa hana jeraha lolote.



Chapisha Maoni

0 Maoni