Nileteeni haraka taarifa ya kuuawa Kibao- Rais Samia

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza kuletewa haraka taarifa ya tukio baya la kuuawa kada wa CHADEMA Mzee Mohamed Ali Kibao pamoja na na mengine ya namna hiyo.

Rais Samia ametoa kauli hiyo kupitia akaunti zake za mitandao ya jamii, kufuatiwa kutekwa na kuuawa kwa Mzee Kibao ambaye mwili wake ulipatikana eneo la Ununio jijini Dar es Salaam.

“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao,” ameandika Raus Samia na Kuongeza “Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.”

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi, amesema Rais Samia.

Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii.


Chapisha Maoni

0 Maoni