Mkuu wa
Oparesheni Kikosi cha Usalama barabarani nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP) Nassoro Sisiowaya akiwa na wajumbe wa Kamati ya Usalama barabarani Mkoa
wa Mbeya alifanya ukaguzi wa kushtukiza kwa madereva wa mabasi ya abiria
yanayofanya safari zake kati ya Mbeya kupitia barabara ya Chunya.
Katika
ukaguzi huo jumla ya Mabasi ya Abiria 03 yalikamatwa, kukaguliwa na kubainika
kuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mfumo wa breki, ubovu na kuzidisha
abiria. Madereva wa vyombo hivyo walichukuliwa hatua mbalimbali ikiwemo kupigwa
faini na kurejesha nauli kwa abiria ili kutafutiwa usafiri mwingine.
0 Maoni