Donald Trump anusurika tena kuuawa Jumapili

 

Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump yupo salama, baada ya jaribio la kutaka kumuua akiwa kwenye uwanja wake wa gofu huko Florida Jumapili mchana, na mtuhumiwa wa tukio hilo anashikiliwa na polisi.

Walinzi maaluma wa viongozi Secret Service waliona mtutu wa silaha ukichomoza kwenye kichaka na kufyatua risasi kuelekea kwa Trump, maafisa wamesema. Trump alikuwa umbali wa mita 275 hadi 455 wakati huo Shirika la Ujasusi la FBI limesema.

Shuhuda mmoja ameripotiwa akisema mtuhumiwa ambaye ametambulika kwa jina la Ryan Wesley Routh aliibuka kwenye nyasi na kuingia kwenye gari aina ya Nissan baada ya walinzi kumfyatulia risasi mara kadhaa.

Maafisa wa usalama walipiga picha namba za gari hilo la mtuhumiwa alilotoroka nalo na kisha baadae gari hilo kusimamishwa katika kaunti ya Martin County, kusini mwa klabu.

Imeelezwa kwamba mtuhumiwa huyo wa jaribio la kumuua Trump jana Jumapili alikuwa mwanaharakati anayeiunga mkono nchi ya Ukraine dhidi ya Urusi.

Julai 13, Trump alinusurika tena kuuawa akiwa kwenye mkutano wa hadhara huko Butler, Pennsylvania baada mtu mwenye silaha Thomas Matthew Crooks kumfyatulia risasi iliyomkosa na kukwaruza sehemu ya sikio lake la kulia.

Chapisha Maoni

0 Maoni