Ajali ya lori la mafuta na lori la mizigo yaua watu 50

 

Watu wapatao 50 wamekufa katika jimbo la kati la Niger nchini Negeria, baada ya lori la mafuta kugongana na lori lililokuwa limebeba watu na ng’ombe na kulipuka moto.

Wakala wa Kusimamia Majanga ya Dharua ya Jimbo la Niger, imesema ajali hiyo imetokea Jumapili na kusababisha mlipuko uliopelekea moto kuzingira magari yote mawili.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Majanga Abdullahi Baba-arah, amesema vikosi vya uokoaji vimepelekwa katika eneo la tukio kutoa msaada.

Katika ajali hiyo pia kuna magari mengine yameungua moto.

Chapisha Maoni

0 Maoni