TLS waamua ni Wakili Mwambukusi Rais wao mpya

 

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimemtangaza Wakili Boniface Mwambukusi kuwa rais mpya wa chama hicho baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi.

Mwambukuzi amepata ushindi wa kura 1,274 ambazo ni sawa na asilimia 57.4, huku ikielezwa misimamo na ujasiri wake umechangia kumpatia ushindi huo.

Uchaguzi huo uliofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kiwete (JKCC) Jijini Dodoma, umefanikiwa kumchagua Mwambukusi kumrithi Harold Sungusia aliyemaliza muda wake.

Chapisha Maoni

0 Maoni