Rais Samia Suluhu Hassan amempongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala
ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff kwa kazi nzuri
inayofanyika nchini.
Rais Samia ametoa pongezi hizo jana alipozungumza na wananchi wa Berega
wilayani Kilosa mara baada ya kufungua daraja la Berega lililojengwa na TARURA.
“Nimpongeze sana sana Mhandisi Seff, wataalam na timu yake
ndani ya TARURA kwa kazi nzuri wanayoifanya Tanzania nzima, nimemvisha maua
yake,” alisema Rais Samia.
Amesema daraja hilo litasaidia kuwaunganisha wananchi lakini
kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.
Pia, Rais Samia amewataka wananchi kutunza daraja hilo, kwa
kuwasihi wasichimbe mchanga ili liweze kutumika miaka mingi.
“Wananchi mnaharibu mazingira, fanyeni shughuli zenu kwenye mto lakini msiharibu mazingira msichimbe mchanga kwenye mto huu, daraja hili limechukua fedha nyingi ili wananchi mnufaike, tunzeni daraja hili,” alisema Rais Samia.
Na. Mwandishi Wetu
0 Maoni