Mwenge wa Uhuru waikubali miradi ya Tsh. 3.5 bilioni Musoma

 

Mwenge wa Uhuru umekagua miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) na kuikubali miradi yote baada ya kuridhika nayo.

Miradi hiyo yote saba iliyokaguliwa ni ya ujenzi wa shule (miradi 2), zahanati, na barabara. Mingine ni ya usambazaji wa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria (miradi 2) na kikundi cha vijana (uchumi).

Mwenge wa Uhuru ulipokelewa kwa shangwe nyingi Jumatano, 31.7.2024 kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) yenye Jimbo la Musoma Vijijini.

Wananchi wa Musoma Vijijini pamoja na Mbunge wao Prof. Sospeter Muhongo wametoa shukrani nyingi za dhati kwa Serikali inayoongozwa vizuri na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.




Chapisha Maoni

0 Maoni