SMZ imevuka lengo la Ilani ya CCM katika viwanda- Dkt. Mwinyi

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imevuka malengo ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 , ambapo ilani ilisema kupima maeneo ya viwanda na kuyaweka tayari  Serikali imetekeleza kwa kupima maeneo hayo, kutayarisha miundombinu ikiwemo ya barabara na miradi ya ujenzi wa  viwanda tayari imeshainiwa.

Dkt. Mwinyi aliyasema hayo alipoweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa eneo maalum liliotengwa na Serikali kwa ajili ya viwanda, Dunga Mkoa wa Kusini Unguja jana tarehe 7 Agosti 2024.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema tayari viwanda viwili vya dawa vimeshatiwa saini leo na vingine vya magari vinakuja katika maeneo ya Dunga.

Vilevile ameeleza kuwa akimaliza awamu ya uongozi mwaka 2025, Serikali itakuwa imeacha alama kwa kukamilisha ujenzi wa viwanda Unguja na Pemba.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali ina dhamira ya kuhakikisha maeneo yaliyotengwa kwa viwanda yanawekewa miundombinu muhimu ikiwemo barabara, umeme, maji, na tehama ili kuvutia wawekezaji wa viwanda wa ndani na nje ya Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi amesema mradi wa viwanda una faida mbalimbali ikiwemo fursa za ajira kwa vijana, kuongeza thamani kwa mazao ya wakulima na wafugaji pamoja na mapato ya Serikali kupitia kodi mbalimbali.

Chapisha Maoni

0 Maoni