Rais Samia aweka jiwe la msingi kwenye mradi wa Suluhu Sports Academy

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan leo August 22,2024 ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Suluhu Sports Academy iliyojengwa na wadau wa Maendeleo wakiongozwa na CRDB Foundation.

Ndani ya Suluhu Sports Academy kutakuwa viwanja vya michezo mbalimbali ikiwemo uwanja wa mpira wa miguu wenye uwezo wa kuchukuwa watazamaji 20,000.

Awamu ya kwanza ya ujenzi wa Academy hiyo inatarajiwa kukamilika Mwezi Aprili mwakani.

Uwekaji wa jiwe la msingi ni sehemu ya shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi Festival 2024.

Chapisha Maoni

0 Maoni