Mchezaji apewa kadi nyekundu kwa kukojoa uwanjani

 

Mchezaji wa timu Atletico Awajun amejikuta akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonekana kama anajisaidia haja ndogo nje ya uwanja wakati wa mchezo huko Peru.

Mshambuliaji huyo wa Atletico alinaswa na kamera akionekana anajisaidia haja ndogo akingojea kupiga mpira wa kona, wakati kipa wa timu pinzani akiwa anatibiwa.

Licha ya mshambuliaji huyo kuzipa mgongo kamera, akitazama eneo lisilo na watazamaji, wachezaji wa timu ya Cantorcillo FC walimshtua refa na ndipo refa akampa kadi nyekundu Munoz.

Maafisa wa Shirikisho la Soka la Peru na wa timu ya Atletico Awajun hawajazungumzia lolote kuhusiana na tuhuma za Munoz.

Chapisha Maoni

0 Maoni