Rais Samia ahudhuria hafla ya kampeni za Raila AU

 

Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Dkt. William Samoei Ruto wa Kenya, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Amolo Odinga, Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, Rais wa zamani wa  Tanzania Jakaya Kikwete pamoja na viongozi wengine Ikulu ya Nairobi, leo tarehe 27 Agosti, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mhe. Dkt. William Samoei Ruto Rais wa Jamhuri ya Kenya wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Mhe. Raila Amolo Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Ikulu ya Nairobi, leo tarehe 27 Agosti, 2024.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mhe. Raila Amolo Odinga akiongea kwenye hafla ya Uzinduzi wa Kampeni yake ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa (AU), Ikulu ya Nairobi, leo tarehe 27 Agosti, 2024.

Chapisha Maoni

0 Maoni