Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii ( NSSF), utaendelea
kukusanya deni la gharama za la Nyerere Kigamboni hadi hapo utakapo rejesha
fedha za mfuko kiasi cha shilingi bilioni 344 ilizotumia hadi kukamilika kwake
kwa kipindi cha miaka 30.
Hayo yameelezwa bungeni leo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile
aliyetaka kujua ni lini NSSF itakamilisha makusanyo ya deni la ujenzi wa Daraja
la Nyerere Kigamboni na kulikabidhi Serikalini.
Mhe. Majaliwa amesema mfuko wa NSSF ulianza rasmi uendeshaji
wa Daraja la Nyerere Kigamboni mwezi Mei 2016 ambapo hadi kufikia mwezi Julai
2024 sawa na miaka Tisa (9) ya uendeshaji, jumla ya shilingi bilioni 102.18
zimekusanywa kutokana na tozo mbalimbali.
”Fedha kiasi cha shilingi bilioni 344 hizi ni gharama za uwekezaji pamoja na ulinzi na thamani ya fedha iliyowekezwa. Hivyo baada ya fedha hizo kurejeshwa mradi utakabidhiwa Serikalini,” ameeleza Mhe. Majaliwa.
0 Maoni