Ndege yaanguka Brazil na kuua watu wote 61

 

Ndege ya shirika la Voepass iliyoanguka katika jimbo la Sao Paulo nchini Brazil imeua watu wote 61 waliokuwamo kwenye ndege hiyo.

Ndege hiyo yenye injini mbili ilikuwa ikitokea Cascavel jimbo la kusini la Parana kwenda uwanja wa ndege wa Guarulhos katika Jiji la Sao Paul ilipoanguka kwenye mji wa Vinhedo.

Picha za kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha ndege hiyo ikianguka huku ikizunguka katika hali ya kupoteza uelekeo.

Ndege hiyo ATR 72-500 ilikuwa na abiria 57 pamoja na watumishi wa ndege wanne. Mamlaka za nchi hiyo zimesema hakuna mtu aliyenusurika.

Chapisha Maoni

0 Maoni