Nataka bima kwa watu wangu wote- Rais Samia

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kuhakikisha wanawafikia wananchi wote ili wawe ndani ya mfumo wa Bima ya afya.

Rais Samia ametoa maagizao hayo leo August 08,2024 wakati akitembelea Maonesho ya Nane Nane kitaifa mkoani Dodoma, ikiwa ni kilele cha Siku ya Nanenane.

"Nataka bima kwa watu wangu wote, nitawaita tuzungumze na nyinyi (NHIF)," alisema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hivi karibuni, Mhe. Rais akiwa ziarani mkoani Katavi na Rukwa kwa nyakati tofauti alihamasisha wananchi kukata Bima ya afya ili wawe na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wote.

Chapisha Maoni

0 Maoni