Mwanamieleka akamatwa Paris kwa kumshika makalio msichana

 

Mchezaji wa mieleka wa Misri Mohamed 'Kesho' Ibrahim anayeshiriki michuano ya Olimpiki amekamatwa Jijini Paris kwa shambulizi la ngono.

Waendesha mashtaka wametoa taarifa kuwa Kesho amekamatwa Agosti 9 majira ya saa 11 alfajiri mbele ya Mgahawa wa OZ.

Inaelezwa kwamba Kesho amekamatwa kwa tuhuma za kushika makalio ya mteja mmoja alitekuwa kwenye mgahawa huo.

Hata hivyo, Kamati ya Olimpiki ya Misri imetoa taarifa ikisema Kesho ameachiwa baada ya kukosekana ushahidi wa kumshika makalio msichana anayemtuhumu.

Chapisha Maoni

0 Maoni