Mhe. Majaliwa amwakilisha Rais Dkt. Samia msiba wa mke wa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo wakati alipohani msiba wa Jokha Hassan Omary ambaye ni Mke wa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Nachingwea mkoani Lindi, Agosti 24, 2024.Waziri Mkuu alitoa pole kwa Niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Wanafamilia, ndugu, jamaa na waombolezaji wote kutokana na msiba huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwenye msiba wa Jokha Hassan Omary ambaye ni Mke wa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Nachingwea mkoani Lindi Agosti 24, 2024. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa mkono wa pole Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman, kwenye msiba wa Jokha Hassan Omary ambaye ni Mkewe, Nachingwea mkoani Lindi Agosti 24, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa heshima za ya mwisho kwenye msiba wa Jokha Hassan Omary ambaye ni Mke wa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Nachingwea mkoani Lindi Agosti 24, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Chapisha Maoni

0 Maoni