Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa Majaliwa amefungua Maonesho ya 30 ya Wakulima, Wavuvi na Wafugaji,
"Nanenane" amanyo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma na kupongeza Wizara
mbalimbali ikiwemo Wizara ya Maliasili na utalii kwa ushiriki kwenye maonesho
hayo.
Waziri Mkuu Majaliwa, amesema maonesho hayo yanaumuhimu
mkubwa kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa na mwananchi mmoja mmoja hivyo ametoa
wito kwa wananchi kutembelea maonesho hayo hayo ili kujifunza na kupitia fusra
mbalimbali zitakazo wainua kiuchumi.
Aidha, katika maonesho hayo, Banda la Wizara ya Maliasili
limesheheni washiriki mbalimbali zikiwemo taasisi zake pamoja na wadau wake,
kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanaotembelea banda hilo wanapata hudama
stahiki kuhusu Uhifadhi na Utalii.
Pamoja na mambo mengine katika Banda la Maliasili na Utalii,
wananchi watapata fursa ya kujua
shughuli za uhifadhi, vivitio vya utalii vilivyopo nchini, kushuhudia vivutio
vya utalii mbashara kutoka hifadhi ya Ngorongoro shughuli za upandaji miti, uanzishaji wa mashamba ya
ufugaji wa Wanyamapori, kuona
wanyamapori hai, makumbusho inayotembea,
na shughuli mbalimbali za Wizara ya maliasili na utalii2 pamoja na
taasisi zake.
Kauli mbiu ya Maonesho ya nanenane mwaka huu ni "Chagua viongozi bora wa Serikali za mitaa kwa maendeleo endelevu ya Kilimo, mifugo na Utalii.
0 Maoni