SGR kufungua fursa za utalii na uwekezaji Kanda ya Kati

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Mradi wa Kimkakati wa Reli kwa Viwango vya Kimataifa (SGR) Kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma yenye urefu wa kilomita 722.

Kufunguliwa kwa Reli hii kutachochea shughuli za kiuchumi, hususani katika sekta za Utalii, Viwanda, Kilimo, Ufigaji na Biashara.

Haya yameelezwa katika hafla ya uzinduzi wa Reli hiyo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, mkoani Dodoma mnamo 01.08.2024.

Katika kuhakikisha fursa hizi zinafahamika ndani na nje ya Nchi, Bodi ya Utalii Tanzania -TTB imeshiriki katika hafla hiyo kupitia uwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu, Bw. Ephraim B. Mafuru ambaye ameeleza kuwa TTB imejipanga kikamilifu kutumia fursa hii ya uwepo wa Reli ya Kisasa kufungua Utalii wa Jiji la Dar es Salaam, mikoa ya Morogoro, Dodoma na Kanda ya Kati kwa ujumla. #TanzaniaUnforgettable.

Chapisha Maoni

0 Maoni