Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi,
akiongoza Kikao cha Mashauriano cha Vyama vya Siasa Wanachama wa Kituo cha
Demokrasia Tanzania (TCD), ambacho, mbali ya viongozi wa vyama hivyo, pia
kilihudhuriwa na mawaziri na manaibu waziri wakiwakilisha upande wa Serikali.
Baadhi ya viongozi wakuu wa vyama hivyo walioshiriki kikao
hicho ni pamoja na Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Ndugu Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Chadema, ambaye
pia ni Mwenyekiti wa TCD kwa sasa, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi (CUF), Ndugu Dorothy Semu, Kiongozi wa Chama cha ACT
Wazalendo na Ndugu Joseph Selasini, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR -
Mageuzi.
Upande wa Serikali, uliwakilishwa na Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Afya, aliyemwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Festo Ndugange, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Mhe. Daniel Sillo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi akifurahia jambo pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe baada ya Kikao cha Mashauriano cha Vyama vya Siasa Wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kilichofanyika leo tarehe 18/08/2024.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba akiongea na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi huku Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akisikiliza baada ya Kikao cha Mashauriano cha Vyama vya Siasa Wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kilichofanyika leo tarehe 18/08/2024.
0 Maoni