Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.
Nape Moses Nnauye (Mb) amekutana na wanahabari kutoka Jumuiya ya Wanahabari wa
Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) ambapo amewaasa kutumia vizuri majukwaa
yao ya habari mtandaoni kujipatia kipato kukuza maisha yao.
Waziri Nape ameyasema hayo alipokutana na wadau wa jumuiya
hiyo tarehe 5 Julai, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam ili kujadili mambo mbalimbali ambayo
yanahusu kuboresha tasnia ya habari mtandaoni.
“Tunafuatiliwa na watu wengi mtandaoni na wengi wanatuamini,
wanatuelewa ninachotaka kuwaomba ni kwamba ni vizuri tutumie mitandao hiyo
vizuri kwa sababu tuna nchi ambayo tuna wajibu wa kuilinda na kuendelea kuwa
katika utulivu wajibu huo ni wetu sote”, alisema Waziri Nape.
Aidha, aliitaka jumuiya hiyo kama wanahabari kutimiza wajibu wa kufichua maovu huku ikitimiza wajibu wa kuilinda nchi, pia aliwataka wanahabari kujikita katika utaalam wa maeneo mbalimbali ili kuweza kuandika habari katika maeneo hayo.
0 Maoni