Waziri Mkuu na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa
leo Julai 03, 2024 amezungumza na wakazi wa kijiji cha Mmawa kilichopo katika
kata ya Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi.
Akizungumza na Wakazi hao Mheshimiwa Majaliwa amesema Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kufikisha huduma za jamii
ikiwemo Afya, maji, Umeme na Elimu katika maeneo yote nchini.
“Kwa mfano katika Wilaya ya Ruangwa na Nachingwea tuna mradi
mkubwa wa maji wa shilingi bilioni 119, kwa mradi huu maeneo mengi hapa
yatapata huduma ya maji. Rais Dkt. Samia pia aliamua kununua mitambo ya
kuchimbia visima vya maji lengo ni kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji
kwenye maeneo yetu.”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka maafisa kilimo nchini kuweka mpango wa kuwahamasisha na kuwasimamia vijana kuingia katika kilimo cha bustani kwenye maeneo ya mabonde yanayofaa kwa kilimo.
0 Maoni