Papa Francis amtunuku Palium Kardinali Rugambwa

 

Papa Francis amemtunuku Palium Mwandhama Protase Kardinali Rugambwa wa Jimbo Kuu la Tabora, Tanzania pamoja na makardinali na maaskofu wakuu wengine kwenye sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo  Mitume.

Adhimisho la Misa Takatifu limefanyika Basilika la Mt. Petro, Vatican. Palium (kitambaa cha sufi) ni mmoja ya ishara ya muunganiko kati ya Askofu Mkuu wa Roma (Papa) na Maskofu wakuu wa Kanda (Metropolitani) ulimwenguni.

Picha maalum kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Vatican Mh. Hassan Iddi Mwamweta na Balozi wa Tanzania nchini Italia Mh. Dr.  Mahmoud Thabiti Kombo. Vatican Inajiandaa kwa Jubilei, 2025.

Chapisha Maoni

0 Maoni